Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб UCHUNGU ANAOPATA MTU PINDI ANAPOFIKWA NA UMAUTI PART 2 в хорошем качестве

UCHUNGU ANAOPATA MTU PINDI ANAPOFIKWA NA UMAUTI PART 2 3 года назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



UCHUNGU ANAOPATA MTU PINDI ANAPOFIKWA NA UMAUTI PART 2

UCHUNGU ANAOPATA MTU PINDI ANAPOFIKWA NA UMAUTI PART 2 Shukrani ni za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), swala na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) Aali zake, sahaba zake na wote wenye kufuata uongofu na njia yake. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mcheni Mwenyezi Mungu na mumuogope, mutii amri zake msimuasi, mumshukuru msimkufuru, mumkumbuke msimsahau. Na mjue kwamba mwanaadamu ameumbwa aishi umri wake, kisha marejeo yake yawe kwenye shimo jembamba akapumzike humo au akaadhibiwe hadi siku ya malipo. Mwanaadamu akiishi maisha haya katika hali ya kutii amri za Mola wake, akitaraji rehma zake na kuogopa adhabu yake, Mwenyezi Mungu humsalimisha na yale anayoogopa na kumtimizia yale anayotaraji, na kwa hiyo roho yake inapotoka huambiwa: { يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ المُطْمَئِنَّةُ ، ارْجِعِي إِلَى رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً ، فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ، وَادْخُلِي جَنَّتِي } [1](Ewe nafsi yenye kutua! Rejea kwa Mola wako hali ya kuwa umeridhia na umeridhiwa. Haya ingia katika waja wangu, uingie katika Pepo yangu)Na huyo hupumzika na huzuni za dunia na shida zake. Ama akiishi katika hali ya kumuasi Mwenyezi Mungu s.w. na kupinga amri zake basi ni maangamivu na shida iliyoje itakayompata! Huyo mpe habari ya kauli ya Mwenyezi Mungu s.w. :{ وَلَوْ تَرَى إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ المَوْتِ وَالمَلاَئِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنْفُسَكُمُ اليَوْمَ تُجْزَونَ عَذَابَ الهُوْنِ بِمَا كُنْتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللهِ غَيْرَ الحَقِّ وَكُنْتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ } [2]((Na kama ungewaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na malaika wamewanyoshea mikono yao (wakiwambia): "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu idhalilishayo kwa vile mlivyokuwa mkisema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo kweli na vile mlivyokuwa mkizifanyia kiburi aya zake)Hivyo mtu dhalimu anapofikwa na mauti na roho ikafika kwenye koo huwa ameshatoka katika kipindi cha kufanya kazi na ameshaingia katika kipindi cha malipo; kwani anayekufa kiama chake huwadia na huyaona kwa macho yake yale yote aliyokuwa akikaidi na kubisha. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Hakika adhabu ya kaburini ni kweli na hakika watu watapewa mtihani makaburini mwao, kisha kaburi huwa ama bustani kati ya mabustani ya Peponi kwa kila muislamu mcha Mungu, au shimo kati ya mashimo ya Motoni kwa kila kafiri na muovu. #UCHUNGUANAOPATAMTUPINDIANAPOFIKWANAUMAUTI #mawaidhayamauti #sikuyakiama #peponimotoni #uchunguwakifo #uchunguwaumauti Na hayo ndio maisha ya barzakh, ambayo kipindi chake ni baina ya mtu kutolewa roho duniani hadi kurudishiwa tena roho wakati litakapopulizwa baragumu la kuhuishwa watu na kutolewa makaburini. Kati ya dalili za kuwepo adhabu ya kaburini ni kauli ya Mwenyezi Mungu s.w. kuhusu Firauni na watu wake: { النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا } [3](Moto wanachomewa asubuhi na jioni)Yaani baada ya wao kuangamizwa kwa kuzamishwa roho zao zinachomwa moto kila siku mara mbili: asubuhi na jioni mpaka siku ya kiyama. Moto unaokusudiwa katika aya hii ni moto wa kaburini na sio moto wa Jahannamu; kwasababu Mwenyezi Mungu s.w. anasema mwishoni mwa aya hiyo: { وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ العَذَابِ } 3((Na siku kitakaposimama kiyama (kutasemwa): "Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali zaidi"))Vile vile kauli ya Mwenyezi Mungu s.w. kuhusu wanafiki wa zama za Mtume s.a.w. waliokuwapo katika mji wa Madina na vitongoji vyake: { سَنُعَذِّبُهُمْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَى عَذَابٍ عَظِيمٍ } #Uchunguwamautinasakratilmauti [4](Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa)Katika aya hii Mwenyezi Mungu s.w. ametaja kwamba wanafiki hawa wataadhibiwa mara mbili kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa. Hivyo adhabu ya mara ya mwanzo ni ya duniani, kwa kuwafichua na kuwadhalilisha, au kwa kuwaletea msiba, au kwa kuwatilisha adabu maalumu alizozipanga kwa makosa maalumu. Adhabu ya mara ya pili ni ya kaburi, na adhabu kubwa ambayo watarudishiwa ndio adhabu ya Moto baada kufufuliwa siku ya kiyama. Vile vile Mwenyezi Mungu s.w. ameyaelezea maisha ya starehe katika kipindi cha barzakhi kwa wale waliokufa mashahidi akasema: { وَلاَ تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ، فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللهُ مِنْ فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِمْ مِنْ خَلْفِهِمْ أَلاَّ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ } [5]((Na usidhani kamwe kuwa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu; bali wahai, wapo kwa Mola wao wanaruzukiwa. Wanafurahia aliyowapa Mola wao katika fadhila zake, na wanawafurahia wale ambao bado hawajaungana nao, walio nyuma yao (duniani), kwamba hakutakuwa na khofu juu yao wala hawatahuzunika)) Na kama Mwenyezi Mungu alivyowaneemesha hawa waliofuzu kwa maisha ya starehe katika kipindi cha barzakhi, basi Yeye pia ni muweza wa kuwafanya wale waliokosa waishi maisha ya adhabu makaburini mpaka kiyama kitakaposimama.

Comments