Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб Fid Q feat Gifted - Glory (Lyric Video ) в хорошем качестве

Fid Q feat Gifted - Glory (Lyric Video ) 2 месяца назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



Fid Q feat Gifted - Glory (Lyric Video )

Glory Lyrics Fid Q Nilikua kama DIRA.. sina kazi baada ya chombo kutia nanga/ au kama TIBA.. sikuwa na mchongo baada ya mgonjwa kukata kamba/ MSHUMAA uliozimwa baada ya machweo kutanda/ SHUJAA aliyeminywa.. wenye vyeo waweze tamba.. nilitupwa kama pingu ya mfungwa alityetoka jela/ Au fimbo ya kipofu baada ya mpofu kuiona hela/ au mkono wa mzazi baada ya mtoto kujua kutembea/ Nilisuswa kama boya mbele ya wajuaji wa kuogelea/ nilishiwdwa kila vita.. nilipigika kama mjinga/ Sikuwahi kuamini, kuna siku na Mimi wataanita bingwa/ Wenzangu ikaanza kuwalipa.. mbona kwangu miamala haisomi? / Nikaumiza kichwa ili mipango isigome/ Wakiweka milima Mimi ninaigeuza vitonga/ Hata nusu hatua ni hatua.. mdogo mdogo nikawa ninasonga/ Japo ni kwa mwendo wa kinyonga/ Mbegu ili kuchipua lazima ioze kwanza mjomba/ Mtaani ninakuta wana wananisemasema siwezi/ Ndani yangu ninasikia sauti inaniambia jamaa unaweza Anguko lina herufi sita, MUAMKO linazo pia/ Huzuni ina herufi sita.. FURAHA inazo pia.. Hook: Gifted: Utukufu ni wako baba..Sifa zote unastahili/ Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi Verse 2: Fid Q: Niilijihisi kama.. koroboi lilozimwa mida ya machweo/ Fukofuko lilotoswa kiwavi ageuke kipepeo/ Maswali yaliyokwisha baada ya elimu kupatikana/ Sikujua. mapito niliyopita ni kipimo cha uungwana/ Niliachwa kama kiota,ndege alipojua kupaa/ Mateso hayakua ajali,bali ni mzani wa ushujaa/ Nilikua ninanuka.. haukuona kinyaa/ Ulininyanyua nikanyanyuka.. sasa kila kona ninang’aa / Niliyoyapitia yalionyesha nguvu niliyonayo/ Majaribu yakauibua ujasiri niliopewa na Mayo/ Nikawa hodari.. nikaweza kuukabili utata/ Ndoto niliyokua nayo imegeuka uhalisia sasa/ Umefanya nijiamini pasina kuweka chembe ya uoga.. nimekubali/ Nilihitaji nianguke, ili ninyanyuke nikiwa ngangari/ Nisikate tamaa au kuhofia/ KUJIKATAA ina herufi tisa.. KUJIAMINI inazo pia.. Hook: Gifted: Utukufu ni wako baba Sifa zote unastahili.. Sio leo tu, hata jana.. umeonyesha unanipenda mimi

Comments