Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video) в хорошем качестве

AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video) 1 год назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video)

STORY BEHIND #NITAAMBATANA Yakiwa yamebaki masaa machache wimbo #Nitaambatana uwe hewani. Leo Ijumaa saa 19:00 yaani saa moja usiku. NAOMBA NIKUSHIRIKISHE SABABU YA WIMBO HUU ILIYO NYUMA YAKE. Tarehe 15 April 2018 Nilipata neema ya kufunga ndoa na Jaqualine Mushi kwa kipindi hicho sasa Jaqualine Mwasongwe,. Tulikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2013 tar 4 November siku ya birthday yake, akiwa Mbeya mwaka wa Kwanza chuo cha Mzumbe akisoma Baf (Bacherol of Accounting and Finance) Mimi wakati huo nilikuwa nasoma Diploma Chuo cha uhasibu Mbeya Tia Pia nikifanya DA (Diploma in Accountacy). Tulianza vizuri mahusiano yetu na baada ya wiki moja tu presha, misukosuko majaribu yaliibuka toka kila pande, lakini tulisimama kwa msaada wa Mungu hatimaye baada ya miaka mitano yaani Mwaka 2018 Ndipo tukafanikiwa kufunga ndoa, Jaqualine akiwa ameshamaliza Degree yale 2016 nami nikifuatia mwaka mmoja baadaye yaani 2017. Tarehe 15 April 2023 Jumamosi tutakuwa tunatimiza Miaka mitano ya ndoa, Unaweza ona tuna miaka 10 tangu tumekuwa kwa mahusiano miaka 5 ya uchumba na 5 ya ndoa. Hili kwetu sio jambo dogo hata kidogo, ni jambo kubwa na zito sana ambalo hatujaliacha lipite tu kimyakimya bila kukumbuka na kufanya kitu ambacho kitakuwa baraka, kumbukumbu, na SHUKRANI ZETU KWA MUNGU. Tukihesabu tuliyosikia, tuliyopitia, tuliyotenda, tuliyotendewa, tuliyosemwa na kusema tunabaki tunashangaa is imekuwaje tumefika hapa? Jibu ni moja tu BWANA AMETUSAIDIA. Sisi hatuna kitu cha kujivuna wala kujivunia tunayaona maisha yetu, furaha, amani upendo, vitu, watu, ndugu, uhai, afya nk Tumepewa tu kwa neema Kwa nini tusimshukuru Mungu kwa haya? TUMEANDAA WIMBO #NITAAMBATANA kama zawadi yetu kwa wanaondoa wote, na wale watakaowa na kuolewa mwaka huu, watakaochumbia na kuchumbiwa na watakaobariki ndoa zao... Huu ni wimbo wenu sisi tumewawakilisha tu. TUNATAMANI SANA WIMBO HUU UPIGWE KWENYE HARUSI YAKO NA UKAWE BARAKA NA MANENO YA WIMBO HUU YAKAWE MAOMBI YENU NA KIAPO CHENU KWA MUNGU. Mkifanya hivyo tutakuwa sehemu ya furaha yenu na tutakuwa sehemu ya familia yenu pia. Mungu awabariki sana na ninaamini utaenda kuupokea wimbo huu kwa furaha na amani tele. Tunawapenda sana. Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe:    • Ambwene Mwasongwe All Music Videos   Follow Ambwene Mwasongwe Instagram:   / ambwenemwasongwe_   Subscribe to Ambwene Mwasongwe:    / @ambweneobadiamwasongwe   Digital Branding & Marketing By: Black Ozen Entertainment Limited:   / blackozenentertainmentlimited   #AmbweneMwasongwe #Nitaambatana

Comments